Thursday, August 20, 2009

SPIKA SITA SHUJAA

SPIKA SITA SHUJAA WA DEMOKRASIA BUNGENI WANAOMPINGA NI MAADUI WA NCHI.
“TUNAHITAJI SPIKA ASIYEKUWA NA CHAMA”
Kumekuwa na taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari juma hili juu ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wajumbe wa kamati kuu ya Chama hicho (CC) kutaka kumwengua uanachama wa CCM na kumvua madaraka spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Samwel Sita ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki kwa tiketi ya chama hicho.

Sababu zilizoelezwa na wajumbe hao ambao hata hivyo wengi wao hawakutajwa moja kwa moja majina yao kutokana na usiri wa vikao hivyo vilivyofanyika Dodoma,ni spika kuishambulia serikali kwa hoja ya kupambana na ufisadi huku akikidhoofisha chama (CCM),hafuati taratibu za mabunge ya jumuiya ya madola huku wengine wakitoa hoja kwamba spika Samweli Sita amekuwa akilitumia bunge kwa kuingilia hoja kishabiki badala ya kuviacha vyama vya siasa vipambane kwa hoja.

Wajumbe wa vikao hivyo vya juu vya CCM walionukuliwa na vyombo vya habari kumshambulia Sita kwa jazba walidai pia kuwa ana kundi lake bungeni linalokadiriwa kuwa na wanachama kumi na mmoja maarufu kama first eleven ambao amekuwa akiwapanga kutoa hoja zinazowalenga watu fulani na pia kuikosoa serikali bungeni kwa malengo binafsi.

Kufuatia malumbano haya yanayogusa hisia za watanzania na hasa kwa kuzingatia umuhimu wa uwakilishi wa wananchi katika chombo muhimu kwa utungaji wa sheria na hata utetezi wa maendeleo ya kiuchumi,kijamii na kisiasa kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC) kinalaani hali hiyo ya kumsakama spika wa bunge kwa tuhuma mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuingilia vipengele vya sheria kama ibara ya 100 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayotoa fursa kwa wabunge kuchangia hoja bungeni bila kuwekewa mipaka.

Wabunge wote wana uhuru wa kusemachochote bungeni kwa maslahi ya watanzania wanao wawakilisha.Spika kwamfumo wa Westminster ambao ndio bunge letu linaufuataanapaswa kutokuwa na upande wowote bungeni, na jukumu lake hasa likiwani kusimamia mijadala yoyote inaendana na katiba ya nchi.Na hakunakikundi au sheria yoyote itakayoondoa uhuru huo.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya bunge watanzania wameshuhudia bunge likisimama kama chombo kitetezi kwa wanyonge na maslahi ya taifa kwa kutetea hoja zenye manufaa kwao kama vile mikataba ambayo hulenga kuwanufaisha wachache na kuliingizia hasara taifa kwa mfano mkataba wa Richmond,sakata la Buzwagi na mengineyo.

Katika haya tumemshuhudia spika Sita akitetea haki ya wananchi kama spika na aikitumia uhuru wake wa kutoa mawazo kama Samweli Sita(binafsi).Hoja za kumpunguzia makali Spika zinakuja baada ya bunge kuonekana msumari kwa wanaotaka kutumia vibaya fedha za umma,hili linatoa tafsiri kwamba amegusa penyewe na kwamba wachache wenye maslahi yao binafsi wanataka kuendelea kujinufaisha.

Ni rahisi kujiuliza kwanini spika aliyetangulia Pius Msekwa hakukumbana na haya? Kwa hoja hizi za wajumbe wa NEC na CC inaonyesha wazi kwamba Msekwa ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa CCM bara alilinda maslahi ya wachache wenye lengo la kujinufaisha kwa kupitisha matakwa yao bila hata kuruhusu yahojiwe na wabunge wenye haki kimsingi kufanya hivyo kwa maslahi ya taifa bila kujali itikadi za vyama vyao.

Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaweka bayana kwamba ili mtu awe mwakilishi wa wananchi katika bunge lazima atumie chama fulani cha siasa kilichosajiliwa.Ndiyo maana bunge letu limesheheni wabunge Kutoka vyama mbalimbali lakini hiyo haitoi fursa kwa bunge kuwa la chama fulani kama CCM hata kama kinaongoza kwa idadi ya wabunge kwani bunge ni la watu wote kwa maslahi ya waatanzania wote wenye itikadi mbalimbali za siasa dini na mengineyo.


Kwa mujibu wa taratibu za uongozi wa kikatiba (Constitutionalism) pamoja na democrasia ya vyama vingi, Mkutano wowote wa chama hauna uwezo wa kumuwajibisha mbunge au Spika wa Bunge kwa maamuzi au matamko yaliyofanyika ndani ya Bunge.Bunge lina uhuru na wabunge wanakinga kwa shughulizi zozote ndani ya bunge ilimradi wasiende kinyume na katiba.Hivyo basi NEC CCM na kamati kuu (CC), imekiuka katiba ya nchi kwa kuwawajibisha wabungeakiwemo spika kwa sababu ya umakini na uwazi wao wanapo kuwa bungeni.Uhuru na kinga kwa wabunge wanapokuwa bungeni haiwezi kuondolewa na sheria yoyote ile isipokuwa bunge lenyewe na katiba ya nchi.

Je CCM wamepata wapi mamlaka ya kuwawajibisha wabunge na Spika aliyechaguliwa na bunge lenyewe tena la vyama vyingi? Tokea lini chama kikawa na mamlaka ya Kumuondoa spika wa bunge?
NEC CCM ,imekosea na iwaombe radhi watanzania wote, kwa kutokujalimichango ya wabunge hao bungeni pamoja na kutokujali misingi ya kidemokrasia na kikatiba na utawala wa sheria.

Kwa hoja hizo hatuna budi kumpongeza spika kwa ujasiri wake wa kutanguliza mbele maslahi ya taifa na kumpa nafasi nyingine aongoze bunge na Si
kumkejeli,kumshambulia, kumzodoa na kumtisha.

No comments: