Monday, December 20, 2010

MALI ASILI YAGEUKA LAANA LOLIONDO

MALIASILI YA YAGEUKA LAANA LOLIONDO
Na Onesmo Olengurumwa.
Loliondo
Kwa ufafanuzi wa haraka haraka mali asili inaweza kutafsiriwa kama rasilimali ambazo Mungu amewajalia wanadamu kulingana na maeneo na mazingira yao. Unapozungumzia mali asili unazungumzia vitu kama mafuta ambayo upatikana zaidi katika nchi za kiarabu, uoto wa asili kama vile mapori na mbuga,wanyama pori ambao upatikana zaidi maeneo yenye wafugaji kama Tanzania na madini ambayo Tanzania imebarikwa kwa kuwa na madini mbalimbali kama dhahabu na Tanzanite.

Tafiti zangu nying zinaonyesha katika sayari yetu hii mali asili badala ya kuwa Baraka kwa jamii zilizotunza na zinazoishi na rasilimali hizo imegeuka kuwa laana kwao.Hii inakuwa laana kutokan na utaratibu mbovu wa usimamizi wa rasilimali hizi, pia inatokan na haki za msingi za wananchi hao kupuuzwa na kuvunjwa na serikali kuwakumbatia wachache kw maslahi ya wachache.Hatimaye mazingira kama haya huwafanya wanachi wazidi kufukarika zaidi huku wachache wakineemeka na rasilimali za nchi.Mwishowe tumeona umwagaji wa damu na machafuko mengi baada ya wananchi kuamua kupigania haki zao za msingi.

Dunia Kuna maeneo mengi ambayo mali asili kama mafuta, madini , misitu na ardhi yamegeuka kuwa laana badala ya Baraka kwa wananchi kwa sababu mbamlimbali.Sababu moja kubwa ni wananch waliotunnza na wanaozunguka rasilimali hizo kuupuzwa na pengine kutengwa kabisa na neema hizo.Eneo la Mto Delta huko nchini Nigeria ni mfano mzuri kuutumia kama sehemu ambayo mali asili imegeuka kuwa laana badala ya Baraka.Damu nyingi umwagika kwa kile kinachoitwa kupigania haki ya kumiliki mali na kunufaika na mali zao zitokanazo na mto Delta.Nchini Sudan hali si shwari pale Darfur au kusini mwa Sudan, pia hapa napo ni laana itokanyo na mali asili.Kujiridhisha zaidi tembelea Jamhuri ya watu wa Kongo uone jinsi mali asili ilivyogeuka kuwa laana na maafa kwa taifa lile lenye utajiri wa madini ya kila aina.Kwa udadisi zaidi angalia mashariki ya kati na jaribu kuchnguza kwa undani nini hasa chanzo cha migorogoro isiyokwisha.

Hapa hapa kwetu katika migodi ya madini, jaribu kupiga picha za haraka haraka katika migodi kama ya North Mara alafu jipe jibu tuna Baraka au laana.Wananchi wa Tarime wametunza milima ya dhahabu kwa miaka mingi lakini kwa sasa wamevamiwa na kufanywa kuwa maskini wa kutupwa, wamegeuka kuwa kama fisi waliobahatika kumkamata pundamlia mnono na baadaye simba kutokea na kuwanyaganya windo lao na kuwageuza kuwa walamizoga.Hali iliyopo kwenye migodi na maeneo yetu ya mali asili haina tofauti na mfano huo wa simba na fisi.Wananchi wamenyang’anywa rasimali zao na kutupwa pembeni wakikodolea macho na mate yakitiririka midomoni mwao mithili ya fisi anayesuburi mzoga toka kwa simba.
Wananchi wanyonge wamefanyiwa kila aina ya udhalimu, wamefyatuliwa risasi kama wanyama pori wengine wakafa na wengine kuwa vilema.Migodi ya Tanzania watanzania wengi wanauwa kinyamela. Zadi zaidi nyumba zoa zimechomwa moto na kuwafanya wageuke kuwa watu wasion na makazi kwa kile kinachoitwa wanambughuzi mwekezaji, mifano tuliyonayo ni ya Kijiji cha Nyamuma Serengeti na vijij vya Loliondo.
Miaka ya 1950 wananchi wa Ngongoro waliokuwa wakiishi maeneo ya Serengeti ambao kwa sasa ni Hifadhi ya Taifa walirubuniwa na wakoloni na kuhamishiwa maeneo ya bonde la crater na maeneo ya loliondo.Kwa Mujibu wa wazee wa enzi hizo wananchi wa ngorongoro waliahidiwa hawatabuguziwa tena kutokana na kwamba maeneo yao yameshakuwa finyu zaidi.Waliadiwa watapata maendeleo mengi kwa kupitia mchango utokanao na maliasili. Lakini hali ilivyo sasa ni tofauti kabisa, wanachi wanaendelea kufukuzwa kwenye maeneo yao bila kufahamu watakapokwenda, wananchi wananyimwa kuchunga mifugo kweneye maeneo yao ya malisho ili kutoa fursa kwa miungu watu kuendelea kunufaika na rasilimali walizopewa watanzania na Muumba wao.Wananchi hawana maisha bora kabisa, bado asililmia 90 hawana elimu na hawana uhakika wa maisha baada ya mifogo yao kuawawa na ukame.
Wafugaji wanapakaziwa kuwa ndio waharibifu wa mazingira, ilhali ndio watunzaji wazuri wa misitu, mbuga, mito, milima na wanyama katika hifadhi na mbuga zetu.Wamasai wanaheshimu sana mazingira kwa sababu asilimia 90 ya maisha yao hutegemea rasilimali hizo.Sasa iweje leo aharibu rasilimali zinazomfanya aishi.Wamasai hawaitaji kula wanyamapori, hawajengi magorofa, hawachomi mkaa pia hawalimi mashamba makubwa zaidi ya vibustani.Mfano tamaduni hazirusu kukata mti mbichi kwani kufanya hivyo ni kuuwa maisha na malisho ya mifugo.Kwa hali kama hiyo nani mwenye akili timamu atathubutu kuwaita wafugaji wa loliondo waharibifu wa mazingira zaidi ya vibaraka wa mafisadi wanaofaidika na rasilimali za Ngorongoro.

Ni mwendazawazimu gani huyo mwenye njaa kali hadi kuamua kununuliwa ili aeleze umma kuwa kengele za mifugo ndio hufukuza wanyama?Je kati ya kengele za ngo’mbe na madege makubwa yenye uwezo wa kubeba magari zaidi ya kumi na yanayotoa mlio mkuwa unaosafiri umbali wa kilometa 100 yanayotua katikati ya pori tengefu la loliondo ni ipi huleta hofu kwa wanyama na viumbe wengine wakiwemo wanadamu? Bila shaka hata mwanafunzi wa shule ya awali atajibu mingurumo ya midege hiyo mikubwa ndio hufukuza wanyama lakini vibaraka wa wachache wanaonufaika na rasilimali za Ngorongoro watasema ni kengele za ngo’mbe ndio huaa Loliondo.Kwanza sheria za nchi haziruhusu madege makubwa kutua karibu na wnayama lakin suala la loliondo limekuwa juu ya sheria.Watu kama hawa ni walarushwa, wabinafsi, wababaishaji, wauaji,wasio na hata chembe ya huruma na vipandikizi vilivyowekwa kwa ajili ya mapepari wachache.Watu kama hawa hawafai kwenye jamii wanapaswa kusulibishwa kwa lengo la kuinusuru jamii.
Haitoshi vibaraka hao wakaendelea kuzungumzia wasichokijua kwa kusema makundi ya mifugo loliondo hufukuza wanyama.Ngoma isiyo kuhusu husiicheze, je mnajua kuwa wanyama na mifugo ni marafiki(They coexist) , je mnajua wanyama kama pundamilia na wengine wanaowindwa na wanyama wakali hupenda kwenda sambamba na makundi ya mifugo kama njia ya kuimarisha ulinzi wao.Je anajua kuwa mida ya ijioni wanyama wote kama tembo, twiga na punda hupenda kuja kulala karibu na maboma ya wamasai kwa usalama zaidi.Je anajua kuwa wanyama kama nyumbu huwa hawazaalii kwenye mapori bali mbugani kwa ajili ya usalama dhidi ya wanyama wakali.Sasa inakuaje leo mseme wafugaji katika pori tengefu la loliondo huaribu mazalia ya nyumbu.Hakika hakuna lolote mnalowaeleza umma zaidi ya umbumbumbu wa mila na desturi za wafugaji, rudini kwa waliowatuma waambieni kwa sasa hakuna aliyewaelewa, pengine tafuteni hoja nyingine.Inakuwaje leo hii tu ndio wafugaji wawe waharibifu na si huko nyuma.
Asilimia zaidi ya 80 ya ardhi ya Ngorongoro ni ama mbuga.hifadhi au mapito na malisho ya wanyama.Na kwa miaka ming sasa wanyama na mifugo wamekuwa wakila, kunywa na kulala pamoja.Hakuna majangili masaini maana wamasai hawana desturi ya ujangili na wala si wafanya biashara, sasa inakuwaje mseme kuwa wamekuwa majangili wa kuua tembo, je faru wanaoua huko hifadhi ya Serengeti ni wamasai ndio wanausika.Na kama ni majangili leo kingekuwa na mnyama hata mmoja katika maeneo ya wafugaji? Na je wanyama wangethubutu kwenda kula na mifugo au kulala karibu na maboma.
Wafugaji wa Ngorongoro wametunza haina zote za wanyama hata wale hadimu kama faru, lakini baada ya shughuli za utaalii na uwindaji kushika hatamu wanyama wanazidi kupungua na wengine wametoweka kabisa kama faru na mbwa mwitu.Je hii sio laana ya mali asili itokanoyo na dhuluma dhidi ya wenye mali hizi.Hivi kati ya mwekezaji katika pori la loliondo na mfugaji nani kamvamia mwenzake au nani anaiua Loliondo? Eneo la pori tengefu la loliondo lipo ndani ya ardhi ya vijiji, je nani ana ubavu wa kumnyima mwanakijiji asitumie ardhi yake. Je uwindaji na uchungaji kipi hufukuza na kumaliza wanyama, jibu lake watanzania wazalendo watanisaidia kuwajibu.
Mmeona haitoshi tu kupora rasilimali za wanangorongoro sasa mmeona mwaite si watanzania bali wakenya.Roria kuna wajaluo ambao pia wapo Kenya,Tarime kuna wakuria ambao pia wapo Kenya, kigoma na maeneo mengine ya mipakani ni hivyo hivyo pia, sasa inakuwaje wamasai wa loliondo muwaite wakenya? Au kuna mipango ya kuwanyaganya ardhi yao yote na hatimaya kuwafukuzia Kenya.
Wanangorongoro wamebakia kuwa maskini wakutupwa, huku wilaya ya Ngorongoro ikiikusanya zaidi ya billion 50 kila mwaka kutokana na mali asili zilizosheheni wilayani hapa.Je hali kama hi si laana ya mali asili?Wafugaji hawa hawana tofauti na Fisi alienyang’anywa windo lake na Simba, na kila akijaribu walau kumega hata mguu simba hucharuka na kuwararuaraua.Mbaya zaidi mifugo karibu robo tatu ya wanangorongoro mwaka jana ilikufa na maboma kugeuka makaburi kutokana na ukame baada ya kufukuzwa katika maeneo ya kuchungia kipindi cha ukame kwa lengo la kumfurahisha mwekezaji.
Rasilimali za Ngorongoro zinawanufaisha wachache tu, wananchi hawapati fursa yoyote itokanyo uwepo wa rasilimali hizo.Watu wachache wamehodhi hata fursa za ajira katika shughuli za kitalii. Mfano Katika kambi ya mwarabu mabasi na malori siku huchukua watu toka miji ya mbali kabisa kwenda kufanya kazi katika makambi ya wawekezaji na kuwaachaa wanangorongoro bila fursa yoyote.Hii ni tofauti na henzi zile tulipokuwa tunasombwa na malori ya mwarabu kwenda kufanya kazi huko makambani, utaratibu ulitoa ajira kwa vijana wengi wa wilaya hii.Kwa sasa Wanaofanya kazi maeneo hayo ni jamaa, rafiki, wajomba na ndugu wengine wa mabosi na mabenager amboa pia nao wametoka mbali..Wananchi hawapati fursa yoyote hata katika taasisi za serikali kama vile Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ajira na fursa zingine zimekuwa zikitolewa bila kutoa vipaumbele kwa wanangorongoro wenye taaluma hizo.
Ni wachache wamepeta fursa hizo na hao pia ni kutoka sehemu ndogo ya wilaya na si wilaya nzima kwani ni vigumu kumkuta mkaazi wa tarafa za Loliondo na Sale wakifanya kazi katika mamlaka ya Ngongoro.Eneo linguine la kutazamwa zaidi ni Mamlaka hii ya Ngorongoro ambayo imekuwa ikipata fedha nyingi zaid ya biliion 40 kwa mwaka lakini halmshauri ya Nogorongoro haiambulii chochote.Je hii Baraka au laana.Matumizi ya uendeshaji wa Mamlaka ni makubwa mno.Wananchi wanalalamika kuona magari ya kifahari yakitumika kwa wingi ndani ya mamlaka.Mbaya zaidi hata lilie fungu lillokuwa likisomesha sehemu ndogo ya wafugaji wa ngorongoro bila pia kuwagusa wananchi wa tarafa za Loliondo na Sale nazo wamezifuta.Kwa sasa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro haina tena mapato yatokanoyo na mali asili baada ya serikali kuu kupokonya vyanzo vyote wakidai watatuma 20%.Je kweli ni haki hii kwa halmashauri iliyopo ndani ya wilaya tajiri inayo ingiza zaidi ya 50 billion kuwa na mapato yatokanayo na mali asili yasiyofika hata million 20.
Je hii ni Baraka au laana, mmewafukuza toka Serengeti, mmewafukuza katika pori la loliondo, mnaendelea taratibu kuwafukuza toka bonde la crater na maeneo ya Tarafa ya Ngorobgoro,mnampango wa kumega ardhi yao ya vijiji kumtengea mwekezaji ardhi, huko soit sambu mmeuza shamba waliloazimwa TBL kwa makampuni ya utalii na pia mnajiandaa kuuteka mlima lengai na ziwa lake.Je wananchi hawa watiifu na wanyonge waende wapi na wale nini? Kwa hali kama hii ni rahisi kupata jibu kwa nini wanawaita wakenya.
Hakika wanachi wa Ngorongoro ni wavumilivu sana na wanahitaji pongezi.Hawana uhakika wa maisha kwani hawana tena maeneo ya malisho, ukame pia unaendelea kutafuna mifugo yao, hawajasoma na hawawezi kufanya biashara, wanaambiwa wajaribu kulima, lakini watalima wapi kila wakilima vibustani wanaambiwa wanaharibu mazingira.Ama kweli hiki ni kiama cha wafugaji, na ndo maana wengi wao wameamia mijijini kukaa milangoni mwa matajiri na kuwalinda wao na mali zao.Maisha yao nayo mijini ni ya kusikitiksha sana hawana pa kulala zaidi ya barazani na magetini.Je ni nani atajitokeza na kuwaokoa wanyonge hawa kabla hawajafia na kutokomea mikononi mwa wachache wenye roho za chuma na macho ya kikatili yenye kuangalia ni wapi pana shilingi bila kujali roho za wanyonge kama wamasai.Wanataka kuzifuta NGO’s zinazojitokeza kuwaelimisha wananchi kujua haki zao, lengo lao ni kundelea kuona wananchi wanabaki kuwa vipofu wa haki zao ili waendelee kuwanyanyasa zaidi.Lakini tunawakikishieni kuwa hakuna shirika lolote lile litakalo futwa au kupata msuko suko wowote ilmradi wanatambulika kisheria.
Naandika haya nikiwa kama sehemu ya jamii hii inayoelekea kutokomea, wanaopata matatizo ni jamaa na ndugu zetu, Mwalimu Nyerere alitufundisha tuitane ndugu, nami naamini watanzania wote ni ndugu zangu na lazima tujitoe muanga kuwasaidia ndugu zetu.Nayosema sijahadithiwa na wala sijapewa ili nilipwe la hasha, ni ya kweli na mengine nimeashuudia.Baadhi ya wawekazi nilishafanya kazi nao kama kibarua katika pori tengefu la lolionndo.Hivyo tunawajua fika na baadha ya watawala wanaoshrikianao nao kila kukicha pia tumewaona mara kwa mara wakija chikua mafao yao katika viikulu vya kifalme vilivyoko ndani ya pori la Loliondo.Tunahitaji wazalendo wote tusimame na kuikoa jaamii hii nyonge inayoelekea kutoweka katika ardhi waliopewa na mola.
Asante kwa kusoma
Imeandaliwa na Onesmo Olengurumwa Makamu Raisi Umoja wa Wasomi Ngorongoro (NDUSA). Email ndusa2008@gmail.com

No comments: