BILA DEMOCRASIA YA VYAMA VYAMA VINGI NORONGORO HAPATABADILIKA.
Moyoni nina machungu,kuona watanzania wenzangu ndugu zangu tukiangamia katika nchi yetu tuliyopewa na Mola.Ni miaka mingi wanachi wa wilaya ya ngorongro tumeishi na kutunza rasilimali inayotuzunguka.Lakini leo hii tunaitwa wavamizi katika ardhi yetu na nchi.Tumekuwa wakimbizi wa ndani mara baada ya seikali kuungana kibega na Wawekezaji kututimuwa na kutuchomea makazi yetu.Tunauliza tuende wapi,elimu hatuna, hatuna maeneo ya kilimo,hatuna maeneo ya ufugaji, hatuwezi kufanya biashara.Kwanini serikali inashirikianana wawekeza kutunyanyasa katika nchi yetu.Wawekeza wamekuwa miungu watu.Wanatumia pesa kutukamata na kutusweka selo.Wanatumia pesa kutugawa.Nini hatima ya maisha yetu?Tunakuomaba Mola ushuke angalau useme na watawala ili watutambue nasi kama binadamu wengine.Tunawapongeza madiwani wote wanaosimama kidete kufichua ufedhulizi unafanyika Loliondo pamoja na mashirika ya wananchi.Kweli mali asili ni mafuta ya Loliondo kama ilivyo Darfur,Niger Delta,Kivu DRC na Masharaki ya kati.Tumechoka kuona DC pamoja na kamati za usalama pamoja na kamati ya Siasa wilaya wakiwa vinara na watetezi wa udhalimu unaofanyika Loliondo.Wananchi muwe makini katika uchaguzi ujao ,msinunuliwe kwa pesa utakayokula siku moja ukataabika milele.wilaya ya Ngorongoro inahitaji siasa ya vyama vingi ili kutoa viongozi wenye sifa na mapenzi bora na wanachi wao.Hivyo vyama vingine nendeni mkatie chachu ya maendeleo wilaya ya Ngorongoro.Mwisho wale wananchi mliionunuliwa kuahalailsha uvujanji wa haki za watu loliondo,ole wenu dhambi hii itawafuata.
Olengurumwa Makamu M/kiti umoja wa wasomi waishio Ngorongoro(NDUSA)
No comments:
Post a Comment