HISTORIA FUPI YA ONESMO OLENGURUMWA
ONESMO PAUL OLE NGURUMWA ni kijana wa mzee Paul Ngurumwa, amezaliwa mwaka 1980 katika kijiij cha Sakala wilayani Ngorongoro, kwa sasa ana umri wa miaka 28 ,ameoa na ana mtoto mmoja wa kiume , makazi yake yapo katika kijiji cha Sakala. Amesoma shule ya msingi Sakala ,elimu ya secondary ordinary level amesoma katika seminary ya Roman Arusha na badaye akamalizia elimu ya advanced secondary Dakawa Morogoro mwaka 2004.Safari yake ya elimu iliendelea pale alipofaulu na kuchaguliwa kusomea fani ya sheria katika chuo kikuu cha Dar es salaam kwa mkopo wa serikali.Hadi hivi sasa ni mwanafunzi wa sheria mwaka wa mwisho na anategemea kuhitimu degree ya kwanza mwakani mwezi wa tano.
WASIFU WA NDANI
Ni kijana mcha Mungu na mwenye misimamo na mitazamo ya kidini katika mambo mbalimbali.Ni mwanaharakati wa haki za binadamu na mwanafunzi alieyejikita katika sheria na masuala ya haki za binadamuna na za kimataifa.Ana misimamo thabiti pale anapoona haki za binadamu zinapovunjwa.Anauwezo mkubwa wa kusimamia kile anachohamini kama ni sahihi vile anapenda kukosolewa.Ana moyo wa kujituma na kujitoa kwa ajili ya maslahi ya umma, hana ubinafsi na anajali utu wa binadamu: akiamini binadamu wote ni sawa.Ni mkweli na muwazi.Anajiamini na ni mbunifu.Siasa zake ni za kiliberali na anapingana na ubeberu wa kimaghararibi pamoja na ubaguzi wa kiukoo.kikabila,kidini,kirangi,kimajimbo,nk.
WASIFU WA KIUNGOZI NA SHUGHULI MBALIMBALI
Onesmo ni kijana wa mzee alieyekuwa kiongozi aliyeheshimika katika jamii yake ya kimasai na hata nje ya jamii.(laiguanani).Toka utotoni wake alionekana akiwa mzuri katika kuongoza wenzake.Ni kiongozi aliyeonesha umahiri wa uongozi hasa alipoanza maisha ya shule.Aliwahi kuwa kaka mkuu katika shule ya msingi na vile vile aliweza kuchaguliwa na wenzake katika elimu ya sekondari na kuwa Rais wa serikali ya wanafunzi katika Dakawa High school. Pia aliaminiwa na kupewa dhamana ya kuwa mwenyekiti wa umoja wa wanafunzi wa kikatoliki hapohapo Dakawa na hatimaye alitunikiwa cheti cha kiongozi bora.Vile vile, kipindi cha masomo yake aliweza kutunukiwa tuzo mbalimbali,kwa mfano, alipokuwa kidato cha kwanza na cha pili alipewa tuzo za utendaji kazi bora (self –reliance awards) na mwanafunzi aliyeacha historia kwa kufanya vizuri kitaluuma wakati huo.
Kabla ya kujiunga na chuo Onesmo alijitolea kufundisha shule ya secondary Emanyata kwa mwaka mmoja na huko nako aliaminika na utendaji wake unakumbukwa.
Talanta yake ya uongozi kamwe haikuweza kufichika hata alipofika chuo kikikuu kwa mwaka uleule wa kwanza aliweza kuchaguliwa na kuwa katibu mkuu msaidizi wa chama cha wanasheria chuo kikuu cha Dar es salaam.Na baadaye umoja wa wanafunzi wakifugaji kule Dar es salaam OSOTWA walimwamini na kumchagua kuwa mwenyekiti wao.Hapa napo hakukawia kuonyesha umahiri wake katika uongozi wake hasa alipobuni lile suala la kuanzisha kampeni ya kuwasaidia walinzi wa jamii ya kifugaji waliojaa mijini.
Hadi wakati huu yeye ni Rais wa chama cha kutetea haki za binadamu chuo kikuu cha Dar es salaam(University of Dar es salaam Human Rights Association) na mapema tu alipopewa dhamana hiyo chama hiki kimeanza kuwika.Vile kwa kutumia falsafa ya ‘‘ panda mlima huku ukiwavuta na wenzako na sio panda kwanza ndipo uwarushie kamba” ameweza kupewa dhamana ya kusimamia kamati ya ufuatiliaji wa fedha za umma(puplic expenditure tracking survey-PETS) Wilaya Ngorongoro kama Mwenyekiti wa kamati hiyo iliyoundwa na PINGOS.Hapa napo umakini wake ulijiweka wazi pale kazi na taarifa ya Wilaya Ngorongoro ilipotunukiwa cheti cha utambuzi wa kazi bora na Balozi wa Marekani kupitia shirika la Pact Tanzania.Hata hivyo akishirikiana na wenzake walifanikiwa kuunda umoja wa wanataaluma mbalimbali Wilayani Ngorongoro(NDUSA) ambapo Rais wake wa muda ni Ndg.Fema Saideya(Mkazi wa Digodigo) na yeye (Onesmo) ni makamu, kama chombo kitakachotumika kuwaunganisha wanachi na wasomi wa wilaya katika harakati za kupambana na umaskini,rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu wilaya hapa na utawala bora.
Ni mwandishi na mtafiti mzuri na amekuwa akifuatilia mambo mbalimali kama vile ukiukwaji wa haki za binadamu na kutoa kweye vyombo vya habari akiamini kuwa njia mojawapo ya kumaliza udhalimu ni kuweka mambo wazi.
MAHUSIANO
Popote pale anapopita imekuwa ni rahisi kwa yeye kujenga mahusiano mazuri kotokana na karama aliyonayo ya kuweza kuishi na watu wa kada mbalimbali.Uhusiano wake mzuri mara nyingi umekuwa ukigeuka kuwa msaada kwa jumuiya au watu anawaongoza.Mfano kwa kushirikiana na Marafiki za watu wa jamii za Kifugaji pamoja na wengine kutoka Sweden wamefikia hatua ya kuanzisha shirika lisilo la kiserikali(TANZANIA MOBILE ORGANIZATION FOR SOCIO-ECONOMIC RIGHTS AND INTREPRENEURSHIP AMONG INDIGENOUS(TAMOSEREKI) litakalokuwa likitoa huduma za kijasiria mali katika jamii za wamasai,amang’ati,wabarbeig,wasonjo,wairaq nk ili kutoa ajira kwa mwananchi wa rika mbalimbali.
“MAENDELEO HULETWA NA WATU,ARDHI,SIASA SAFI NA UONGOZI BORA”
MWL NYERERE.
No comments:
Post a Comment