TVT KIPINDI TUAMBIE. TAREHE 22 /11/2007
HAKI ZA MSINGI ZA MKIMBIZI.
HISTORIA YA WAKIMBIZI TANZANIA
Tanzania imekuwa ikipokea wakimbizi toka miaka 1960 toka pande mbalimbali takriban nchi kumi ,Ruanda ,Burundi,Somalia,DRC, ,South Africa, Malawi ,Msumbiji,Zimbabwe,.walikuja kwa wingi kutokana na sera ya wakatio huo (OPEN DOOR POLICY). Sera hii ilitokana na FALSAFA YA MWALIMU NYERERE NA BAADHI YA VIONGOZI kwamba mkimbizi yoyote anayekuja kwa mikati ya kuikomboa nchi yake aingie bila masharti ,wakapewa ardhi,wakaishi,wakafanya kazi kama watanzania na bila kutegemea misaada hatimaye wakawa naturally intergrated.Hawakuwa na mzigo wowote katika nchi walizalisha na kufanya biashara na watanzania,mfano kule Rusumo kulikuwa na soko la pamoja na Bulyankulu .sheria ya wakimbizi ya mwaka 1966 (refugee control Act) ilitumika hadi tulipopata sheria mpya ya mwaka 1998.(refugee Act).
Tokea miaka ya tisini chuki dhidi ya wakimbizi ilianza kushika kasi hatimaye baadhi ya viongozi walisikika wakitoa maneno makali dhidi ya wakimbizi ,mfano namnukuhu waziri wa mambo ya ndani katika miaka ya tisini ,
“We are saying enough is enough is enough. let us tell the refugee that the time has come for them to return home and no more should come”
halikadhalika viongozi wa upinzani walitumia nafasi hio kueleza umma kwamba serikali inafanya makosa kuwahifadhi wakimbizi.
MKIMBIZI NI NANI? Ni mtu yoyote yule aliyekosa usalama wa nchi yake kutoakana na na mambo mbalimbali ambayo humfanya awe na hofu kubwa ya ulinzi na usalama wa maisha yake.. kwa mujibu wa sheria ya wakimbizi duniani ya mwaka 1951 kifungu cha 1(2).mkimbizi lazima awe ni mtu mwenye hofu kuu , aliyetoka katika nchi yake na kwenda nchi nyingine kutafuta hifadhi na ulinzi.
Hofu hiyo inayomkimbiza mkimbizi kwa mujibu wa sheria za wakimbizi duniani na sheria inayosimamia masuala ya wakimbizi Afrika ya mwaka 1969 ni unyasasaji wa kidini,kisiasa,kikabila,kirangi na hata utawala wa kimabavu na kikoloni.
Kifungu cha 3 cha cha azimio la kimataifa la haki za binadamu la 1948 kinasisitiza kuwa kila mtu hana haki ya kuishi ,kuwa huru na kuwa salama.Azaimio hilo linaendelea kusema katika kifungu vifungu vya 13 hadi 15 kila mtu ana haki ya kwenda katika nchi yoyote ile na kuomba hifandhi.
HAKI ZA MSINGI
Haki ya kwanza ambayo mkimbizi anapaswa kupata ni haki ya kuomba uifadhi katika nchi ya yoyote bila kuzongwa na masharti magumu.kifungu cha 2(1) cha sheria inayosimamia masuala ya wakimbizi Africa 1967 kinasisitiza kwamba kila nchi itumie mbinu zote kuwapokea wakimbizi.suala la kuwapokea wakimbizi kwa mtazamo huu linabakia kuwa suala kibinadamu zaidi make hakuna sheria yoyote inayolazimisha inchi yoyote kumpokea mkimbizi ila suala la kuomba ukimbizi ni haki ya msingi ya mkimbizi hivyo Tanzania haikufanya na haifanyi makosa yoyote kuwapokea wakimbizi.
Charter ya Afrika ya haki za binamu ya mwaka 1981 nayo imetumia neno kuomba na kupata lakini bado tu imetoa uhuru kwa sheria za nchi kuamua , kifungu 12.3
Haki ya kupata ulinzi kamili.mkimbizi anapokuwa katika nchi ya hifadhi anakuwa chini ya uangalizi wa umoja wa kimataifa hasa chini ya shirika la wakimbizi duniani pamoja nchi ya hifadhi..kifungu ch 7 (1) ch sheri za wakimbizi duniani kinaweka bayana kwamba inchi yoyote inayompokea mkimbizi ni lazima(shall accord) iwalinde na kuwaimarishia usalama wao kama inavyowatendea wageni wengine wanaoshi nchini kisheria kifungu13 cha sheria hiyo kinasisitiza pia.
Mkimbizi hapaswi kurudishwa anapokuwa mpakani au anapokuwa ndani ya nchi anayotaka hifadhi.(priciple of non refaulment) hasa pale nchi yake inapokuwa katika wimbi la machafuko ya kivita. Kifungu cha 33 cha sheria za kimataifa za wakimbizi kinasistiza kwamba nchi yoyote itakayomrudusha mkimbizi katka eneola vita itakuwa imekiuka haki za kibinadamu.vile sheria ya wakimbizi ya Africa kifungu cha 2(3) na kifungu cha 28 cha sheria za wakimbizi Tanzania.
Baada kupata hifadhi mkimbizi vile vile kama binadamu yoyote yule ana haki ya kutendewa kama binadamu yeyote yule kwa mujibu wa sheria za kimataifa za wakimbizi
Ø Haki ya kumiliki mali isiyohamishika na inayohamishika. Kifungu cha13
Ø Haki ya kuwa msanii au kijihushisha na sanaa
Ø Haki ya kujiunga au kuunda vyama vyovyote ilimradi visiwe vya kisisasa kifungu 14
Ø Haki ya kwenda mahakani na kupewa msaada wa kisheria
Kifungu cha 17
Ø Haki ya kujiari na kuajiriwa
Ø Haki ya kupata elimu
Ø Uhuru wa kutembea
Ø Uhuru wa kuabudu
Ø Uhuru wa mawasiliano
Kwa mujibu wa sheria za kibinadamu za kimataifa pamoja na sheria za wakimbizi za kikanda, mkimbizi hana budi kupata haki zote kama binadamu wengine,mfano mkimbizi ana haki ya msingi ya kukata rufaa pale anaponyimwa kibali cha kupata hifadhi.
Pamoja na haki hizo kufafanuliwa na baadhi ya sheria za kimataifa kimsingi bado sheria za kimataifa za wakimbizi zina mapungufu hasa zile za ndani ya nchi. Mfano sheria ya wakimbizi ya kimataifa inamapungufu makubwa na baadhi ya mapungufu hayo ni pamoja ufafanuzi wamkimbizi ni nani bado unamatizo pamoja na kwamba imeshafanyiwa mabadlilko na protoko ya 1967 ya sheria ya wakimbizi.
Vile sheria hii haijaweka bayana haki za msingi za wakimbizi wenye udhaifu(vulnerable) kama vile watoto,wanawake,vikongwe na vilema.
Sheria hii haina uwezo wa kuiwajibisha nchi itakayoshindwa kufuata misingi ya sheria za wakimbizi.kutokana na tatizo hilo tunaona nchi nyingi duniani zikivunja na kukiuka haki za msingi za wakimbizi.
Sera na sheria ya wakimbizi Tanzania kwa ujumla ziinamapungufu makubwa ukizingatia Tanzania ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kupokea wakimbizi nadhani tungepaswa pia kuwa nchi pekee yenye sera na sheria za wakimbizi zinazo jali haki za mkimbizi.
Tatizo la kwanza kabisa ni kwabmba sheria na sera hiyo haitekelezwi ipasavyo na kwa misingi ya kisheria inayojali haki za kibinadamu.(practical problems) Zoezi la kupata kibali cha kuwa mkimbizi lina urasimu ukizingatia kuwa wakimbizi huwa wanafika wakiwa wengi na vile vile wanakuwa wamegubikwa na wimbi la matatizo kifungu cha 5 (2) e) cha sheria za wakimbizi Tanzania.vile vile kifungu cha 9(7) ambacho kinamruhusu mkimbizi kukata rufaa.
Kifungu cha 4.3 kinapingana na sheria za wakimbizi kimataifa na Afrika inayo pinga mkimbizi kurudishwa katika nchi yake bila kuzingatia misingi ya haki za binadamu.sheria za wakimbizi mkimbizi anapaswa kurududishwa kwao kwa hiari yake na hasa pale machafuko yanapokuwa yamekwisha katika nchi ya nyumbani.
Suala la kurudi nyumbani kwa hiari na kwa usalama limekuwa chanzo cha ukiukwakji wa haki za wakimbizi.mfano miaka ya tisini na kitu Tanzania iliwarudisha wakimbizi 20 wa kirundi kwa kigezo cha kuwa ni wapiganaji na hatimaye wakauwa mpakani.ili hali sheria inasema kama kutakuwa na watu wa namna hiyo wanapaswa kutengewa kambi zao. Zoezi hilo kwa wanyarwanda miaka ya1996 walirudishwa kwao shingo upande na hatimaye wenge wao sasa wanatangatanga katika eneo la maziwa makuu kama vile kule Uganda katika makambi ya kibati na nakivale.
Hata hivyo msemaji wa UHCR Ron Redmond alipata kusema (we need to do great rehabilitation and reconstruction for Sudanese back home)
Hivyo basi nchi husika wakishirikiana na shirika la wakimbizi duiniani wanapaswa kujenga mazingira mazuri ya wakimbizi kurudi nyumbani kwa kupata haki zao za msingi manake kuwepo na amani haitoshi tu kuwafanya wao watake kurudi nyumbani.hali kadhalika zoezi la hivi karibuni la kuwarudisha wakimbizi DRC na Burundi halikufuata misingi ya kisheria.
Kifungu cha 28 cha sheria ya wakimbizi Tanzania kina matatizo kwa sababu kina mzunguzia mkimbizi aliepo ndani ya nchi ya hifadhi tu na kumsahau yule atakaekuwa mpakani,kwa maan hiyo mkimbizi alieko mpakani anaweza kurudushswa kinyume na kifungu cha 2.3 cha sheria za wakimbizi Africa na kifungu 33 (1) sheria za wakimbizi za kimataifa.
Tanzani imeweka mazingira magumu (restrictive measures ) ambayo ina mnyima mkimbizi kuwa huru na kufnya kazi.nchi inaweza kufanya hivyo pale tu labda mkimbizi si halali kisheria na hana sifa zifuatazo
Ø lazima awe amekaa zaidi ya miaka 3 katika nchi ya hifadhi
Ø ameoa katika nchi ya ukimbizi
Ø ana watoto katika nchi ya ukimbizi
hivyo sheria yetu inamapugufu kwa kutoweka kipengele cha sheria kinachomruhusu mkimbizi kupata hifadhi ya kudumu kama njia moja wapo ya kutatua tatizo la ukimbizi(naturalization).wakati huo huo vifungu vya 3 na 33 vya Azimio la dunia la haki za binadamu ambayo Tanzania imeiridhia inasisitiza kuwa mkimbizi ana haki ya kubadili utaifa.
Sheria ya wakimbizi Tanzania pamoja na sera ya wakimbizi ya mwaka 2003 bila shaka kunahitajika mabadiliko makubwa kwa maslahi ya nchi vile vile ikizingatia haki za mkimbizi. Mfano Sera ya Taifa ya wakimbizi ya 2003 inasisitiza suala la safe zones kama ufumbuzi wa kudumu wa matattizo ya wakimbi,hili nalipinga kabisa kwa misingi ya kwamba haindani na haki za binamu na ni kinyume na sheri zingine za wakimbizi.ni vigumu kumlazimisha mkimbizi abakie kwenye nchi ambayo anaona maisha yake yapo hatarini.
Labda pendekezo ambalo nadhani ndio linaweza kutoa suluhu ya kudumu katika matatizo ya wakimbizi hasa hasa katika eneo la maziwa makuu ni kuwepo na shirikisho la Afrika mashariki.
IMEANDALIWA NA MWANAHARAKATI HAKI ZA BINADAMU
UDSM
ONESMO P.OLENGURUMWA
6 comments:
I'm interest reading you brother, please send me a refugees right article via my email
I'm interest reading you brother, please send me a refugees right article via my email
Nina mume wang alikua anafuatilia kitambulisho cha taifa jana tar25/2/2020 waka mkamata kwamadai ya kua yeye sio mtanzania baba yake nimtu wa Burundi mama yake nimtanzania mkazi wakigoma na mumewangu kazaliwa kigoma alafu baba ake alikua anafuatilia Chet cha ila Hakija kamilika wamagoma kumuachia na mpaka sasa hiv yuko kituon je yeye anakosa hapo
Ok thanks if you got it please forward to me through jmwilima65@gmail.com
Naomba kuwasiliana na muundaji WA hii taarifa
Asante
Tanzania Hawa heshimu hata kimoja kwa hivi vyote
©Haki ya kutembea
©Haki ya kumiliki mali yoyote
©haki ya kujiajiri
Hizi haki zote hazi heshimiwe,
So naomba Sheria na hukumu mpya za wakimbizi nchini tanzania 2023
Post a Comment